Msuguano
Msuguano ni hali ya kitu kutokukubaliana na mwendo wa vitu vigumu, vitu vya kimiminika na vitu vinavyosuguana vyenyewe.
Kuna aina mbalimbali za misuguano:
Msuguano mkavu ni msuguano wa vitu viwili vyenye asili ya ugumu pamoja. Msuguano mkavu umegawanyika katika msuguano ambao vitu hivyo havina mwendo, na msuguano ambao vitu vina mwendo.
Msuguano kimiminika umeonyeshwa kama msuguano katika mfumo wa kimiminika ambao una mwendo.
Msuguano laini ni kama kwenye msuguano wa kimiminika ambapo vimiminika laini vinaachanishwa na vitu viwili vigumu.
Msuguano wa ngozi ni kitu kinachoenda kinyume cha mwendo wa kimiminika kupitia kwenye mwili.
Msuguano wa ndani ni msuguano unaoenda kinyume na mwendo katikati ya vitu vinavyounda vitu vigumu.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Msuguano kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |