Nicky Byrne
Nicholas Bernard James Adam Byrne (amezaliwa tar. 9 Oktoba 1978 mjini Dublin) ni msanii wa muziki wa pop kutoka nchini Ireland. yeye ni mwanamuziki mkongwe zaidi katika kundi la Westlife la huko nchini Ireland.
Nicky Byrne | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Nicholas Bernard James Adam Byrne |
Amezaliwa | 9 Oktoba 1978 Dublin, Ireland |
Aina ya muziki | Pop |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo |
Aina ya sauti | Tenor |
Miaka ya kazi | 1998–mpaka sasa |
Ame/Wameshirikiana na | Westlife |
Kama mcheza mpira
haririKabla kujiunga na kundi linaloimba muziki wa miondoko ya Sligo lililoitwa alikuwa akicheza mpira wa miguu ambapo alikuwa akicheza katika timy ya Home Farm F.C. na pia timu ya Mtakatifu Kevins Boys F.C. iliyoko kaskazini mwa Dublin.[1] Alikuwa mchezaji mpira kwa taaluma na kujiunga na timu ya Leeds United kama mlinda lango mwaka 1995, na pia alikuwa moja ya wachezaji katika timu iliyoshiriki na kushinda kombe la FA Youth Cup mwaka 1997[2]
Alichezea timu ya Leeds kwa kipindi cha miaka miwili, na kuacha baada ya mkataba wake kuisha mwezi Juni mwaka 1997, alicheza kama mchezaji wa ziada katika mechi ya Scarborough F.C. katika mechi ya majaribio na timu ya Cambridge United kabla ya kujiunga na timu ya mjini mwake ya Dublin club Shelbourne. alisaini mkataba na timu ya Cobh Ramblers na kucheza michezo 11, baadae katika St. Francis F.C., zote zikiwa za kigi za nchini Ireland.[3]
Tarehe 14 Mai, 2009 Nicky alicheza kama mchezaji wa ziada akiwa na timu ya Liverpool FC timu ilicheza na timu ya All Star XI katika eneo la Hillsborough Memorial katika maadhimisho ya jubiliei ya miaka 20, ya Hillsborough disaster.
Muziki kama kazi
haririMwezi Juni 1998, alishiriki katika mashindano ya sauti ya boyband, ambapo mkurugenzi wa kundi la Boyzoneambaye ni Louis Walsh, ambapo Walsh alimfata na kumwomba kujiunga na kundi la Westlife. Hapo alijiunga na kundi hilo pamoja na wenzake Kian Egan, Mark Feehily, Shane Filan na Brian McFadden.
Byrne pia ana nyimbo ambazo zimeshafika katika nafasi ya kwanza mwaka 2002, Albamu yao ya kwanza na kundi la Westlife, ilitoka Mwezi novemba mwaka 1999, iliyoitwa Westlife. Akiwa na Westlife, Brian amashakua na nyimbo 14, zilizofanikiwa kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya muziki ya Uingereza na albamu 7 katika nafasi ya kwanza huku zikifanikiwa kuuza nakala zaidi ya milioni 40 duniani kote. .[4]
Byrne pia maeshiriki katika kutunga mashari ya nyimbo kadhaa akiwa na wanakikundi wenzake, ikiwa ni pamoja na nyimbo za makundi mengine.
Familia
haririAlimuoa rafiki yake wa kimapenzi wa tangu utotoni Georgina Ahern katika ofisi za serikali ya Ireland.[6] Harusi hii ilifuatiwa na sherehe mbalimbali katika siku ya jumamosi tarehe 9 Agasti walifnga ndoa kanisani, katika kanisa la Kikatolokila mtakatifu Petro la Gallardon, Eure-et-Loir, Ufaransa and a reception at the nearby 16th century Château d'Esclimont.[7]
Georgina alipata mapacha wasiofanana wa kiume tarehe 20 Aprili 2007, wiki 6 kabla ya muda wake,[8] The children were christened on 15 Julai 2007 in the Saint Sylvester Church in Malahide, Dublin.[9]
Wazazi wa ubatizo kwa watoto wa Nicky ni dada yake Nick pamoja na mume wake Mark Gallagher.[10]
Diskografia
hariri- Nothing Is Impossible
- Don't Let Me Go
- When You Come Around
- Imaginary Diva
- Reason For Living
- Crying Girl
- You Don't Know
- Never Knew I Was Losing You
- Where We Belong
- Singing Forever
- I Won't Let You Down
- You See Friends (I See Lovers)
- I'm Missing Loving You
Marejeo
hariri- ↑ "www.homefarmfc.ie/news.php". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-15. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.
- ↑ "Nicky Byrne — Biography".
- ↑ "Club History". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.
- ↑ "Westlife line-up spring show".
- ↑ http://www.thecommitted.com/cgi-bin/index.cgi?action=forum&board=MP3s&op=displaysticky&num=11984
- ↑ BBC News. "Westlife star's French wedding" (Website). BBC News. Iliwekwa mnamo 2007-12-22.
- ↑ "Taoiseach becomes grandad to twin boys". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-22. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.
- ↑ Daniel Kilkelly. "Westlife star becomes dad to twins". Digital Spy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (Website) mnamo 2008-12-11. Iliwekwa mnamo 2007-12-22.
- ↑ "Westlifer Nicky Byrne's twin babies are christened".
- ↑ "Bertie's a double winner".
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nicky Byrne kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |