Oksijeni (en:oxygen) ni elementi simetali yenye namba atomia 8 na uzani atomia 15.9994 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni O.

Oksijeni
Oksijeni ndani ya chupa katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto chini ya -182.95 °C
Oksijeni ndani ya chupa katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto chini ya -182.95 °C
Jina la Elementi Oksijeni
Alama O
Namba atomia 8
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 15.9994
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 54.36K (-218.79°C)
Kiwango cha kuchemka 90.20K (-182.95 °C)
Asilimia za ganda la dunia 49,4 %
Hali maada gesi

Ni kati ya elementi zilizopo kwa wingi ulimwenguni ikishika nafasi ya tatu baada ya hidrojeni na heli. Kwenye dunia yetu asilimia 28 za masi yake ni oksijeni; ni elementi iliyopo kwa wingi kabisa katika ganda la dunia.

Hutokea ama kama mchanganyiko wa elementi nyingine au pekee yake kama gesi isiyo na rangi wala herufi. Pekee yake hupatikana hasa kama molekuli ya O2 yaani mchanganyiko wa kikemia wa atomi mbili. Kuna pia oksijeni ambayo ni molekuli ya atomi tatu unaoitwa ozoni (O3).

Umuhimu wake duniani ni hasa kuwepo katika maji na katika hewa ya angahewa na kwa ujumla kwa ajili ya uhai. Karibu viumbe vyote duniani hutegemea oksijeni. Wanaipata ama kwa kupumua hewani au kwa kuichukua kwenye maji. Oksijeni tupu ni sumu kwa ajili ya viumbe vingi.

Kama atomi ya pekee ya oksijeni inakutana na atomi mbili za hidrojeni zinakuwa H2O (maji).

Matumizi ya gesi ya oksijeni

hariri

Gesi ya oksijeni hutumiwa sana katika teknolojia mbalimbali. Kwa sababu mwendo wa kuchoma huhitaji oksijeni inatumiwa pale ambako jota inatakiwa, kwa mfano wakati wa kuchomelea inapochanganywa na gesi ya asetilini.

Vile hutumiwa katika roketi. Injini zote za petroli au diseli huhitaji oksijeni lakini kwa kawaidi zaichukua hewani tu. Oksijeni tupu ina hatari yake kwa sababu yaweza kusababisha mlipuko ikikutana na moto.

Kutengeneza kwa oksijeni

hariri

Hutengenezwa kwa njia mbalimbali hasa kwa elektrolisisi ya maji kuwa gesi ya O2 na H2. Inapatikana pia kwa kuvunja kabonati ya kalsi (CaCO3) kuwa CaO na O2.

Mimea hupata mahitaji yao ya oksijeni katika chanikiwiti kutokana na CO2 na maji kwa nishati ya mwanga wa jua kuwa O2 na C6H12O6 inayojenga molekuli mpya za selulosi.

Sifa za oksijeni

hariri

Oksijeni ina sifa mbalimbali ambazo huweza kuwa za kawaida ama za kikemikali. Sifa hizo ni kama vile

  1. Oksijeni huyeyuka kidogo sana katika maji.
  2. Oksijeni ni gesi yenye densiti kubwa kuliko ile ya hewa.
  3. Oksijeni haina hatua yoyote katika maji ya chokaa.
  4. Oksijeni inasaidia mwako. Ukiweka njiti ya kiberiti inayokaribia kuzima kwenye chombo chenye gesi ya oksijeni, njiti hiyo itaendelea kuwaka.
  5. Oksijeni ni gesi isiyokuwa na harufu, rangi wala ladha yoyote ile.
  6. Oksijeni huchanganyika na madini au metali zisizo za sumu ili kuunda oksidi ya metali au oksidi zisizo za metali.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Oksijeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES