Osiris alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Katika mitholojia ya Kimisri aliabudiwa kama mungu wa uhai, kifo, mafuriko ya mto Nile, na maisha ya baadaye.

Osiris, bwana wa mauti, mwenye taji ya pekee na mwili wa kijani. Muguu yake imefungswa tayari katika kitambaa cha mumia.
Hukumu ya wafu mbele ya Osiris; upande wa kushoto roho inapimwa kwenye mizani

Mitholojia

hariri

Alikuwa kaka na mume wa Isis. Walikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Horus.

Katika masimulizi ya Wamisri Osiris aliuawa na kaka yake Set lakini Isis alifaulu kumrudisha katika uhai. Mama wa Osiris alikuwa mungu wa kike Nut, na baba Geb[1], dada Nephthys, na dada na vile vile mke Isis, jinsi ilivyo kawaida katika familia za Kifalme za Misri ambako mara nyingi dada na kaka walioana. [2]

Mungu mpendwa katika Misri

hariri

Ustaarabu wa Misri ulimheshimu Osiris kama mungu mmojawapo lakini pia kama mfalme wa kwanza aliyedhaniwa kuwa na hekima na upole. Katika masimulizi yao aliwafundisha watu wa Misri kuachana na desturi ya kula nyama ya binadamu na kutoa binadamu kama sadaka; aliwafundisha pia kilimo na utaratibu wa ibada.

Kazi yake

hariri

Osiris alikuwa mungu wa kuzimu. Jukumu moja kama bwana wa kuzimu ilikuwa kufanya hukumu ya mwisho kabisa ya wafu. Katika imani ya Misri, roho iliweza kukubaliwa katika kuzimu lakini wale waliokataliwa walizimika kabisa, ilhali hakuna mafundisho kuhusu adhabu au mateso.[3]. Osiris alihusika pia kuwalinda watu kutokana na hatari zilizohofiwa kutoka kuzimu kwa walio hai.

Mwonekano

hariri

Osiris alichorwa kwenye taswira za ukutani kama farao aliyevaliwa vitambaa vya mumia kwenye sehemu ya chini ya mwili wake. Alivaa taji nyeupe yenye manyoya ubavuni akishika fimbo ya farao. Osiris alionyeshwa kuwa na ngozi ya kijani kibichi, akiashiria kuzaliwa upya kwa Wamisri.

Marejeo

hariri
  1. Wilkinson, Richard H. (2003). The Complete Gods and Goddesses of Ancient Egypt. London: Thames & Hudson. uk. 105. ISBN 978-0-500-05120-7.
  2. Wilkinson, Richard H. (2003). The Complete Gods and Goddesses of Ancient Egypt. London: Thames & Hudson. uk. 105. ISBN 0-500-05120-8.
  3. "Letter: Hell in the ancient world. Letter by Professor J. Gwyn Griffiths", December 31, 1993. Retrieved on 2021-03-20. Archived from the original on 2012-09-01. 

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 17