Paneli ya sola (pia: paneli ya Jua; kutoka Kiingereza: solar panel) hukusanya nishati kutoka Jua kwa matumizi ya binadamu.

Mfumo wa kimsingi wa paneli ya sola

Kuna aina mbili za paneli za sola

  • paneli zinazokusanya joto (thermal)

Paneli ya sola ni tafsiri ya Kiingereza "solar panel". "Solar" inamaanisha kitu kinachohusiana na Jua (kutoka Kilatini sol = Jua); "panel" ni sehemu nyembamba na bapa.

Paneli za kukusanya joto

hariri
 
Paneli za kukusanya joto, pamoja na tangi la maji.

Paneli za jua za joto kawaida hufanywa kutoka kwa sanduku lililofunikwa kwa kioo. Ndani ya sanduku kuna mabomba meusi; rangi nyeusi inasaidia kupokea mwanga wa Jua, ilhali kioo cha juu kinaruhusu miale ya Jua kufika ndani ilhali kinatunza joto ndani ya sanduku.

Katika paneli sahili maji hupashwa moto moja kwa moja; ilhali maji ya moto huwa na densiti ndogo, hivyo ni mepesi kuliko maji baridi, hupanda juu ambako yanaingia katika tangi; maji ya tangi yaliyo baridi zaidi ni mazito yakishuka kuingia katika paneli. Kwa njia hiyo kuna mzunguko wa maji ambayo yanaongezeka joto kwa kila mzunguko. Maji hayo yanaweza kutumiwa bafuni au jikoni.

Paneli tata zaidi hutumia kiowevu cha pekee ambacho kinazunguka kwa msaada wa pampu katika kifaa cha kupitisha joto kwa maji au mafuta fulani. Muundo huo unafaa pia kwa kukanza nyumba katika mazingira baridi maana mafuta au kiowevu cha pekee kinaweza kupita dirishani mwa paneli bila kuganda hata kama jotoridi ya mazingira inashuka chini ya °C wakati wa usiku.

Paneli za nuruumeme

hariri
 
Paneli za nuruumeme kwenye mapaa ya nyumba huko Ujerumani.

Paneli za aina hii huwa na idadi kubwa ya seli za umemenuru ambazo zinabadilisha nishati ya nuru kuwa umeme. Umeme hukusanywa katika beteri na kutoka hapo inaweza kubadilishwa tena kuwa umeme wenye volteji inayotumiwa na vifaa kwenye nyumba.

Paneli nyingi zinazounganishwa zinatoshelezea hata mahitaji makubwa ya umeme kama kiwandani[1]. Mara nyingi umeme kutoka paneli za nyumba moja unaingizwa katika mtandao wa umeme wa kitaifa (gridi).

Matumizi

hariri
  • kuongeza joto la nyumba
  • kuendesha pampu za nguvu
  • kuchaji beteri wakati wa mchana kwa matumizi ya umeme wakati wa usiku
  • kuwezesha nyumba yako, kambi, kabati, kumwaga chombo, au jengo lingine lolote kwa jambo hilo.
  • vituo vyenye paneli nyingi hufanya kazi ya kituo cha umeme.[2]
 
STS-97 ISS paneli za sola kwenye Kituo cha Anga cha Kimataifa

Tanbihi

hariri
  1. ""Solar Power Plant Report"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-06. Iliwekwa mnamo 2019-12-28.
  2. Timothy Thiele. "Top 10 Energy Uses". About Home. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-15. Iliwekwa mnamo Mei 17, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paneli ya sola kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
HOME 1
os 1
web 1