Piza (Kiitalia: pizza) ni chakula chenye asili ya Italia kilichosambaa kote duniani. Ni kipande cha mkate bapa kinachofunikwa kwa mchuzi mnene wa nyanya na vipande vya jibini. Mara nyingi vipande vyembamba vya mboga mbalimbali, nyama au samaki vinaongezwa pamoja na jibini. Yote huokwa katika joko, jibini inayeyuka na kuunganisha sehemu nyingine za pizza.

Pizza "Margerita" ni namna asilia ya pizza kutoka Napoli.
Pizza ya peperoni (=pilipili).
Pizza kubwa namna hii inakatwa vipandeipande.
Pizza inavyookwa katika jiko.

Mwaka 2017 UNESCO imetangaza ufundi wa Wanapoli wa kupika pizza kuwa "urithi wa dunia".

Historia ya pizza

hariri

Mtangulizi wa pizza, na pia chanzo cha jina lake, ni "pita" ya Kigiriki. Tangu milenia watu wa nchi za Mediteranea walitengeneza chakula cha moto kwa kuoka mkate bapa pamoja na majani, mafuta na jibini, pia nyama iliyosagwa. Hii "pita" ya Wagiriki inapatikana pia katika nchi jirani, kwa mfano Uturuki kwa jina "pide".

Pizza yenyewe ina chanzo chake katika mji wa Napoli (Italia kusini) wakati wa karne ya 19. Mwanzoni pizza ilisambaa kutoka Napoli hadi sehemu nyingine za Italia. Baadaye wahamiaji kutoka Italia walileta pizza hadi nchi walipohamia na hapo wenyeji wa nchi hizi walianza kupenda chakula hiki.

Hatua nyingine za usambazaji ilikuwa utengenezaji wake viwandani ambako pizza zinaandaliwa na kugandishwa katika chumba cha barafu. Kama chakula barafu huuzwa kupitia maduka yenye friza na kuokwa katika joko la nyumbani. Kutokana na wingi wa ladha na urahisi wa kuiweka mezani pizza barafu, namna hizi za pizza zinauzwa kwa wingi katika mazingira yenye maduka ya friza.

Nanma ya kutegeneza pizza

hariri

Kinyunga kinatenegezwa kwa kutumia unga wa ngano, maji, chumvi, hamira na mafuta kidogo. Kinyunga kinakaa kwa muda wa angalau saa 1, halafu kinatandikwa nyembamba sana. Hapa ndipo tofauti muhimu na aina za "pita". Kinyunga bapa hufunikwa ama kwa vipande vyembamba vya nyanya au mchuzi mnene wa nyanya uliopikwa pamoja na viungo kama vitunguu saumu na majani yenye ladha; nyanya hufunikwa kwa jibini iliyosagwa au iliyokatwa bapa nyembamba sana. Hapo ndipo pizza asilia inayowekwa katika joko na kuokwa kwa joto kubwa iwezekanavyo, mara nyingi sentigredi 400-500 kwa dakika chache tu.

Kuna namna nyingi kubadilisha na kuongeza ladha ya pizza kwa kuongeza viungo vingine juu na ndani ya kanda la jibini. Mara nyingi vipande vyembamba vya nyama kama soseji, samaki au wanyama wengine wa baharini, uyoga, mboga kama vitunguu, zaituni, pilipili, pilipili hoho na mengine vyatandikwa hapa. Hakuna vyakula visivyoweza kukatwa vyembamba na kutumiwa hapa.

Manufaa ya pizza kwa afya yako

hariri

Rojorojo ya nyanya (tomato sauce) husaidia kupigana na saratani. Rojorojo hii huwa na kiungo cha lycopene ambacho chasemekana pia kusaidia mwili usiwe wa kupata magonjwa kwa haraka.

Inapopikwa vizuri kwa kutumia mboga, proteini na mafuta mazuri, pizza husaidia mwili kukua vizuri na kupata lishe bora.

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pizza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
mac 1
os 5