Remigius au Remi wa Reims, (kwa Kifaransa: Rémi au Rémy; Cerny-en-Laonnois, karibu na Laon, Picardy, 437Reims, Champagne, 13 Januari 533) alikuwa askofu wa Reims (Ufaransa) kwa miaka zaidi ya 60.

Mt. Remigius akimbatiza Clovis I, mchoro wa Master of Saint Gilles, 1500 hivi (National Gallery of Art, Washington, D.C.)
Sanamu ya Mt. Remigius huko Simpelveld, Uholanzi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1][2].

Mafanikio

hariri

Alipata umaarufu kama mtume wa Wafaranki kwa sababu alileta kwa Kristo kabila hilo kubwa la Kigermanik, la kwanza kujiunga na Kanisa Katoliki bila kupitia kwanza Uario. Tarehe 25 Desemba 496 alimbatiza mfalme Clovis I na kwa njia hiyo alivutia Wafaranki wengi katika Ukristo, jambo muhimu sana katika historia ya Kanisa na ya Ulaya kwa kuwa hilo lilikuwa kabila la kwanza la Wagermanik kuingia Kanisa Katoliki bila kupitia Uario halafu lilitawala sehemu kubwa ya Ulaya magharibi na kuunda ustaarabu wake.

Maandishi

hariri

Kati ya maandishi yake, mengi yamepotea[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Great Synaxaristes: Kigezo:Gr icon Ὁ Ἅγιος Ρεμίγιος Ἐπίσκοπος Ρημῶν. 13 Ιανουαρίου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
  2. January 13 Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine.. The Roman Martyrology.
  3. Few authentic works of Remigius remain: his "Declamations" were elaborately admired by Sidonius Apollinaris, in a finely turned letter to Remigius, but are now lost. Cfr. Book IX, p. vii. Four letters survive: one containing his defence in the matter of Claudius, two written to Clovis, and a fourth to Bishop Falco of Tongeren. Cfr. Philip Schaff, "The New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge," entry by A. Hauck

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES
mac 2
os 2