San Juan, Puerto Rico

San Juan ni mji mkuu na mji mkubwa wa Puerto Rico ambayo ni eneo maalum la Marekani kwenye kisiwa hicho cha Karibi.

San Juan
Municipio Autónomo de San Juan
San Juan (mbele: ngome na mji wa kale)
Nchi Puerto Rico, Marekani
Anwani ya kijiografia 18°24′23″N 66°3′50″W / 18.40639°N 66.06389°W / 18.40639; -66.06389
Kimo mita
Eneo km2
Wakazi 395,326 (milioni 2 katika rundiko la jiji)
Msongamano wa watu 3,187
Simu 787 na 939
Tovuti rasmi sanjuanciudadpatria.com/en

Idadi ya wakazi ni 433,733. Ni mji wa 42 kwa ukubwa katika Marekani.

Leo, San Juan ni bandari muhimu zaidi ya kisiwa cha Puerto Rico.

Historia

hariri

San Juan ilianzishwa kama kituo cha Wahispania mnamo 1521, miaka michache baada ya kufika kwao katika Amerika. Ilipokea jina lake kwa heshima la San Juan Bautista, umbo la Kihispania la Mtakatifu Yohane Mbatizaji. Ikawa bandari muhimu, kituo cha kijeshi na cha kibiashara. Kanisa lake lililokamiliswa mwaka 1540 ni kanisa la kale la pili katika mabara ya Amerika. Hadi leo San Juan ina majengo mengi ya zamani bado yamesimama.

Kutokana na uvamizi wa Puerto Rico wa mwaka 1898 katika Vita ya Marekani dhidi Hispania mji umekuwa chini ya utawala wa Kimarekani. Tangu Puerto Rico kupata haki ya kujitawala kama eneo la ng'ambo la Marekani, San Juan inasimamiwa na uongozi unaochaguliwa na wananchi wenyewe.

Utamaduni

hariri

Sawa na Puerto Rico yote, wakazi wengi huongea Kihispania ambacho ni lugha rasmi ya kwanza, pamoja na Kiingereza.

Muziki wa San Juan unafanana na ule ya Karibi.

Ngome ya kale ya Kihispania pamoja na sehemu ya mji wa kale imepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.[1].

Uchumi

hariri

San Juan imeendelea kuwa mji wa tasnia mbalimbali kama vile kemia, dawa za tiba na kilimo, nguo, pombe kali ya rum na elektroniki.

Utalii ni muhimu na mji pamoja na mazingira yake huwa na hoteli nyingi za kila ngazi.[2]

San Juan inahudumiwa na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Luis Muñoz Marín.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu San Juan, Puerto Rico kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1