Shane Steven Filan (amezaliwa tar. 5 Julai 1979) ni msanii wa muziki wa pop kutoka nchini Ireland. Huyu ndiye mwimbaji kiongozi wa kundi la Westlife. Filan ni moja ya waimbaji watano wa asili wa kundi la hili, akiwa na wenzake, Kian Egan, Mark Feehily na Nicky Byrne na aliyekuwa mwenzao Brian McFadden.

Shane Filan
Shane Filan
Shane Filan
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Shane Steven Filan
Amezaliwa 5 Julai 1979 (1979-07-05) (umri 45)
Asili yake Sligo, Ireland
Aina ya muziki Pop
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo
Ala Sauti
Aina ya sauti Baritone
Miaka ya kazi 1998–mpaka sasa
Studio SonyBMG UK/Ireland
Ame/Wameshirikiana na Westlife

Wasifu

hariri

Filan alizaliwa tarehe 5 Julai 1979, wazazi wake wakiwa ni Peter na Mae Filan, alikulia katika eneo la Sligo, mji mdogo katika kaskazini-magharibi mwa Ireland. Akiwa mdogo katika famila yake yenye watoto saba. Filan ana dada watatu na kaka watatua ambao ni Finbarr, Peter Jr, Yvonne, Liam, Denise na Mairead. Wazazi wake wanamili mmghawaha katika eneo la Sligo unaoitwa Carlton uliopo katika barabara ya Castle na Shane amekuwa akifanya kazi hapo kama mhudumu, hasa ilipokuwa naumri mdogo.

Filan amesoma katika chuo cha Summerhill College, ambayo ni shule ya Kikatoliki amesoma na wenzake Kian Egan na Mark Feehily. Wote watotu walishiriki katika kutengeneza bendi ya muziki ya shule, wakati wote wakiwa na miaka 12.Filan anampenda sana Michael Jackson na anasema kuwa, mwanamuziki huyu ndiye aliyemvutia hadi kuamua kuwa mwanamuziki .[1]

Muziki

hariri
Makala kuu: Westlife

kabla ya kujiunga na kundi la Westlife, Egan na Feehily walikuwa na Filan katika kundi lilijulikana kama I.O.U. na waimbaji wengine wa eneo la Sligo, kama vile Derrick Lacey, Graham Keighron na Michael "Miggles" Garrett. Ameshiriki katika kutunga wimbo wa IOYOU.wimbo wa Together Girl Forever. kwa miezi sita, mamaye Shane, Mae Filan, alijaribu kumpigia simu Louis Walsh (ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Boyzone). Hatimaye aliweza kuongea nae kuhusu bendi ya mtoto wake. Watu kati yao waliachwa na wengine watatu yaani Shane, Kian na Mark waliondoka na kuungana na wenzao wawili yaani Nicky Byrne na Brian Mcfadden na kuunda kundi la Westlife

Filan pamoja na Mark Feehily, ndio viongoza katika uimbaji wa kundi la Westlife. Katika nyimbo nyingi za Filan ndiye mara nyingi huanza kuimba. TAlbamu yao ya kwanza ilitoka mwaka 1999 iliyoitwa Westlife.[2]

Filan pia ameshiriki katika kutunga nyimbo mbalimbali akiwa na wenzake.

Maisha binafsi

hariri

Filan amemuoa mpenzi wake wa tangu utoto Gillian Walsh, ambaye ni ngudu wa Kian Egan, jumamosi ya tarehe 28 Desemba mwaka 2003, katika Ballintubber Abbey, na kufuatiwa na sherehe katika jumba la Ashford. nchini Ireland.[3] Wawili hawa wana watoto wawili hadi sasa na wanategemea kupata mtoto mwingine Januari ya mwaka 2010

Diskografia

hariri
  • Fragile Heart
  • Bop Bop Baby (Became a hit single and made it into #5 in U.K. singles charts)
  • I Wanna Grow Old With You
  • Don't Say It's Too Late
  • Love Crime
  • How Does It Feel
  • Crying Girl
  • Reason For Living
  • Miss You When I'm Dreaming

Pia ameandika nyimbo zilizoimbwa ba wasanii wengine kama vile:

  • Listen Girl ulioimbwa na John Ostberg
  • Let Me Be the One ulioimbwa na Casey (wimbo huu umetungwa na Shane mwenyewe)
  • Sei Parte Ormai Di Me ulioimbwa na Il Divo [4]

Marejeo

hariri
  1. Westlife's Shane: I was a Jacko nut. Virgin Media: music news (30 Oktoba 2009). Retrieved on 5 Novemba 2009.
  2. "Dublin Tourism - Concerts & Gigs - Westlife `Back Home Tour' 2008 with Special Guest Star Shayne Ward". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.
  3. "Shane & Gillian Marry in Mayo..." ShowBiz Ireland. 2003-12-29. Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
  4. "Sei Parte Ormai Di Me by Il Divo - Rhapsody Online". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-30. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shane Filan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES