Shayiri
(Hordeum vulgare)
Shayiri
Shayiri
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama nyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Hordeum
Spishi: H. vulgare

Shayiri (kutoka Kiarabu شعير; kwa Kiingereza: "barley") ni mmea wa familia ya nyasi katika ngeli ya monokotiledoni.

Mbegu au punje za shayiri ni nafaka.

Kihistoria ilikuwa chakula muhimu cha watu, lakini siku hizi hulimwa zaidi kama chakula cha wanyama.

Hata hivyo inaungwa katika mkate na ni sehemu ya chakula cha kawaida cha watu katika nchi za Ulaya ya Mashariki.

Inahitajiwa pia kwa ajili ya vinywaji mbalimbali kama bia au maji ya shayiri inayopendwa huko Japani.

Kwa jumla shayiri inavumilia chumvi katika ardhi kuliko ngano lakini haivumilii baridi kama aina kadhaa za ngano.

Walimaji wakuu wa shayiri (2005)
 Nafasi  Nchi  Mavuno 
(kwa t elfu)
 Nafasi  Nchi  Mavuno 
(kwa t elfu)
   1 Urusi    15.773    9 Marekani    4.620
   2 Kanada    12.133    10 Hispania    4.448
   3 Ujerumani    11.722    11 Denmark    3.730
   4 Ufaransa    10.357    12 Poland    3.461
   5 Ukraine    9.000    13 China    3.350
   6 Uturuki    9.000    14 Uajemi    2.900
   7 Australia    6.640    15 Ucheki    2.280
   8 Uingereza    5.545     Dunia    139.044

Utangulizi

hariri

Shayiri ni zao la nafaka, linalotokana na nyasi zikuazo kwa mwaka, ‘Hardeum vulgare’. Siku hizi shayiri hutumika hasa kulishia mifugo, huku kiasi kidogo kikitumika kutengenezea vileo (bia na vinywaji vingine) na kwenye chakula chenye nguvu. Shayiri hutumika kwenye supu, michemsho na mikate katika nchi mbalimbali kama vile Uskoti, na Afrika.

Mnamo mwaka 2007, kulingana na takwimu za mazao ya nafaka duniani, shayiri lilikuwa zao la nne kwa wingi wa tani milioni 136, ukichukua kilometa za mraba 560,000.

Kadiri ya biolojia, mmea wa shayiri ni miongoni mwa familia ya nyasi. Hujichavusha wenyewe, wenye kromosomu 14. Ni uzao wa nyasi za porini, Horeum vulgare wa spishi ya spontaneum. Inapatikana kwa wingi kwenye maeneo yenye nyasi na miti midogo, na hupatikana hata kwenye maeneo yaliyotumika/haribiwa, pembezoni mwa barabara na mashamba makubwa. Mbali na hapo hupatikana kwa nadra sana.

Makazi

hariri

Shayiri-pori huwa na masuke yenye uwezo wa kupasuka; na pindi inapokomaa masuke hupasuka na kusambaa na kusaidia kutawanyika kwa mbegu. Shayiri inayolimwa mashambani ina masuke yasiyopasuka na kusambaa, na kufanya iwe rahisi kuvuna masuke yaliyokomaa. Aina hii ya shayiri inayopasuka ni matokeo ya kuchanganya uzazi wa shayiri jamii mbili tofauti.

Shayiri zilizo na zisizo na maganda: Shayiri zisizo na maganda/zilizowahi ni shayiri zenye maganda ambayo ni rahisi kutoka. Ni mazao ya zamani, lakini sasa yamevuta makini ya viwanda vingi na matumizi yake yameongezeka, hasa kwa kiasi cha kingi cha mashati, hasa kwa nguruwe na kuku. Pia shayiri hii imechunguzwa kama inaweza kutumika yote kama punje nzima na matumizi yake kwenye nusa na makapi.

Historia

hariri

Shayiri ndiyo nafaka ya kwanza kuanza kupandwa huko Mashariki karibu na wakati ambao ngano nayo ilipoanza kutumika. Shayiri pori ilipatikana kuanzia kaskazini mwa Afrika mpaka Krete upande wa Mashariki, na mpaka Tiet kwa upande wa Mashariki.

Ushahidi wa shayiri pori wa mwanzo kabisa ni ule kutoka Epipaleolithic huko Ohalo kusini mwa Bahari ya Galilaya, mabaki yanayokadiriwa kuwa ni ya kabla ya 1700 KK.

Shayiri ya kawaida ya mwanzo kabisa ilipatikana huko Mashariki ya Kati, Syria.

Inatajwa mara kadhaa katika Biblia: maarufu zaidi ni tukio linalopatikana katika Injili la Yesu kuzidisha mikate ya shairi pamoja na samaki kwa ajili ya umati mkubwa wa watu.

Shayiri ililimwa kwenye peninsula ya Korea tangu 1500-850 KK pamoja na mazao mengine kama mtama, ngano na jamii ya mkunde.

Bia ya shayiri pengine ndiyo kinywaji cha kwanza kuwahi kutengenezwa na watu wa Neolithic. Baadaye shayiri ilitumika kama fedha. Pamoja na ngano, shayiri ikawa chakula kikuu huko Misri, ambako ilitumika kutengenezea mikate na bia. Katika dini, hasa jamii za zamani, shayiri ilitumika kama zao kuonyesha haki.

Katika Uingereza wa zamani, mikate ya shayiri ilionekana ikitumiwa na watu wa hali ya chini (wakulima) huku wale walio katika ardhi ya juu hula mazao mengine ya shayiri na si mikate.

Viazi vilichukuliwa nafasi yake na shayiri mnamo karne ya 19.

Ulimaji

hariri

Mmea wa shayiri huweza kukua sehemu mbali mbali. Hakuna hasa maeneo ya joto la kawaida ambako hulimwa kama zao la kiangazi na maeneo ya tropiki ambako hupandwa kama zao la kipupwe. Hulimwa baada ya siku 1-3. Shayiri hupenda kukua katika hali ya baridi, lakini haitishiwi sana na mazingira ya baridi.

Shayiri huvumilia sana udongo wa chumvichumvi kuliko ngano, na hii huweza kuelezea sababu ya shayiri kulimwa kwa wingi sana huko Mesopotamia kutoka milenia ya pili KK na kuendelea. Lakini shayiri hushindwa kuvumilia baridi kama ilivyo kwa ngano ya kipupwe (Thicum, aestivum), lakini huweza kupandwa kama zao la kipupwe kwenye maeneo yenye joto kama vile Australia.

Shayiri huwa na msimu mfupi wa kuku na kuvumilia ukame.

Uzalishaji

hariri

Shayiri ilikuwa inakuzwa kwenye nchi takribani 100 duniani mwaka 2007. Mnamo mwaka 1974, mavuno ya dunia nzima yalikuwa tani 148,818,870 na kisha hapo yamekuwa yakipungua.

Matumizi

hariri

Kulisha wanyama, nusu ya shayiri inayolimwa Marekani hutumika kulishia mifugo. Shayiri ni chakula cha mifugo kwa maeneo mengi duniani na hasa maeneo ambayo hayawezi kukuza mahindi, hasa kaskazini mwa Ulaya. Hutumika pia huko Kanada.

Kutengeneza vileo; kiasi kikubwa cha shayiri hutumika kuchemsha pombe, ambapo shayiri huwa chaguo sahihi. Ni viungo muhimu kwenye uzalishaji wa bia na wiski.

Vinywaji vya shayiri visivyo na kilevi, kama vile maji ya shayiri na chai ya shayiri (inayoitwa mugisha huko Japan), hutengenezwa kwa kuchemsha shayiri kwenye maji. Mvinyo wa shayiri kilikuwa ni kilevi cha miaka 1200, na kiliandaliwa kwa kuchemsha shayiri kwenye maji, na kisha huchanganywa na mvinyo na viungo vingine kama limau na sukari viliongezwa. Kufikia mwaka 1800, mvinyo mbalimbali na sukari vilikuwa vinatengenezwa kutoka viungo vya Kigiriki.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shayiri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1