Sifaka
Sifaka taji
Sifaka taji
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota (Viumbe walio na seli zenye kiini)
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda: Strepsirrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na lemuri)
Oda ya chini: Lemuriformes (Wanyama kama kima)
Familia ya juu: Lemuroidea (Lemuri)
Familia: Indriidae (Lemuri walio na mnasaba na indri)
Jenasi: Propithecus
Bennett, 1832
Ngazi za chini

Spishi

Sifaka (kutoka Kimalagasi: sifaka) ni spishi za lemuri wa jenasi Propithecus katika familia Indriidae. Kama lemuri wote wanatokea Madagaska tu. Jina lao linafanana na sauti yao: “shi-fak”. Manyoya yao ni marefu na laini kama hariri. Rangi yao ni nyeupe, kahawia au nyeusi au muunganisho wa rangi hizi. Uso wao ni mweusi. Mwili wa wanyama hawa una urefu wa sm 40-55 na uzito wao ni kg 3-6. Urefu wa mkia ni sawa na mwili. Hula majani, maua na matunda.

Spishi

hariri

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

  NODES
Idea 1
idea 1
mac 2
os 2