Sophie Okonedo (alizaliwa London, 11 Agosti 1968) ni mwigizaji wa filamu na televisheni, na msimuliaji wa filamu wa Uingereza.

Okonedo alianza kazi ya filamu katika drama ya nchini Uingereza ambayo inaitwa Young Soul Rebels (1991). Baadaye, Okonedo aliigiza kwenye filamu ambayo inaitwa Ace Ventura: When Nature Calls (1995), na baadaye katika filamu za Dirty Pretty Things (2002) na Hotel Rwanda (2004).

Maisha ya mapema

hariri

Sophie Okonedo ni binti wa Joan, mwanamke wa Kiyahudi ambaye alizaliwa katika eneo la London mashariki, na Henry Okonedo (alizaliwa mwaka 1939 - alifariki mwaka 2009), Mwingereza mwenye asili ya Nigeria. Mama yake, Joan, alikuwa mwalimu wa mazoezi ya viungo yaitwayo ‘pilates’, na baba yake, Henry, alikuwa mwajiriwa wa serikali.

Wakati yeye alipokuwa na umri wa miaka mitano, baba yake aliacha familia yake na alirudi katika makazi yake ya zamani mjini Lagos, Nigeria. Kwa sababu baba yake aliacha familia yake wakati Sophie alipokuwa mdogo sana, yeye hakujifunza sana kuhusu baba yake wala utamaduni wa baba yake kutoka Nigeria. Baada ya baba yake kuacha familia yake, Okonedo alilelewa na mama yake tu. Yeye alilelewa kujifunza kuhusu dini ya mama yake, Uyahudi.

Wao waliishi na ufukara kwa miaka mingi. Sophie na mama yake waliishi Chalkhill, makazi ya umma yaliyoko London kaskazini ambayo yalikuwa na ufukara sana, vurugu, na uhalifu. Wakati Sophie alipokuwa kijana, mara kwa mara watu walimtendea vibaya kwa sababu alikuwa mwanamke mweusi na alikuwa na mama mweupe. Sophie alikuwa na huzuni na mkanganyiko mara kwa mara. Kwa sababu watu kutoka pande zote walimbagua, Sophie hakujisikia kuwa karibu na utamaduni wa Kiyahudi wala wa Kinigeria wakati yeye alipokuwa kijana.

Kazi yake

hariri

Okonedo alisoma katika Chuo cha sanaa ya drama kiitwacho ‘Royal Academy of Dramatic Art’. Yeye alifanya kazi katika vyombo vya Habari vingi, kama vile filamu, televisheni, na maigizo ya sauti. Mchezo wa kuigiza wa kwanza ambao maarufu sana wa Okonedo unaitwa Hotel Rwanda. Ile filamu ilitoka katika mwaka 2004, na yeye aliigiza kama Tatiana Rusesabagina, mke wa meneja wa hoteli ya Rawanda na mwanaharakati wa masuala ya kibindadamu, Paul Rusesabagina. Kwa sababu yeye alikuwa na nafasi hiyo, yeye akawa mwanamke wa pili mweusi mwenye asili ya Uingereza kupokea uteuzi wa Tuzo ya Academy “Academy Award” kwa mwigizaji msaidizi wa kike kwenye Tuzo za Academy za sabini na saba katika mwaka 2005. Baadaye, Okonedo alipokea uteuzi wa tuzo ya Golden Globe kwa mfululizo wa kipindi cha televisheni ambacho kinaitwa Tsunami: The Aftermath (2006) na tuzo ya BAFTA ya televisheni teule kwa mfululizo wa kipindi cha televisheni ambacho kinaitwa Criminal Justice (2009) na filamu ambayo inaitwa Mrs. Mandela (2010). Filamu nyingine ambazo yeye anajulikana pia kwa kuigiza inaitwa Aeon Flux (2005), Skin (2008), The Secret Life of Bees (2008), na Christopher Robin (2018).

 

Maisha binafsi

hariri

Okonedo ana binti mmoja, kwa uhusiano wa zamani na mwendeshaji filamu Eoin Martin. Binti wa Okonedo anaitwa Aoife na alizaliwa katika mwaka 1997. Leo, Okonedo anaishi na binti yake Aoife katika nchi ya London ya kaskazini.

Marejeo

hariri
  • Burack, E. (2019, March 19). 18 things to know about Sophie Okonedo. Alma. Retrieved October 19, 2021, from https://www.heyalma.com/18-things-to-know-about-sophie-okonedo/.
  • Encyclopedia.com. (2021, October 21). Sophie Okonedo Biography. Encyclopedia.com. Retrieved October 18, 2021, from https://www.encyclopedia.com/education/news-wires-white-papers-and-books/okonedo-sophie.
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sophie Okonedo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 3