Spam
Spam ni neno la Kiingereza linalomaanisha usambazaji wa idadi kubwa ya habari zisizotafutwa na wapokeaji, hasa kwa njia ya intaneti, baruapepe na njia nyingine za kidijitali. Watu wanaosambaza spam mara nyingi huitwa kwa neno la Kiingereza "spammer".
Asili ya neno
haririKiasili "spam" ilitaja aina ya nyama ya nguruwe iliyouzwa tangu 1936 katika kopo, ikiwa kifupi cha "SPiced hAM". Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa nyama ya pekee iliyopatikana kwa urahisi nchini Uingereza hata kama watu hawakuipenda sana. Upatikanaji huu ulisababisha mizaha mingi kuhusu "spam" na kati ya hii ni hasa filamu fupi ya waigizaji wa vichekesho "Monthy Python" inayoonyesha wateja katika mgahawa ambako kila chakula kinaandaliwa na spam[1]. Tangu miaka ya 1980 neno hili lilianza kutumiwa pia kwa marudio ya habari,hasa matangazo ya kibiashara, kwenye ngazi za awali za intaneti[2].
Baruapepe za spam
haririBaruapepe za spam ni umbo la kidijitali za matangazo ya kibiashara yanayosambazwa kwa wingi yakilenga watu ambao hawakuomba kuyapokea. Baruapepe za spam hutumwa kwa anwani nyingi iwezekanavyo kwa shabaha ya kuwahamasisha wapokeaji kununua bidhaa au huduma, au kutangaza maoni fulani. Mfumo wa kutumia baruapepe umesambaa sana kwa sababu ni gharama ndogo kuzituma kwa wingi.
Biashara ya anwani
haririMaspammer huwa na changamoto kupata anwani nyingi. Hapa ni chanzo cha biashara ya data za watu. Thamani ya anwani inaongezwa kama inaunganishwa na data kuhusu mahali mtu anapoishi, kazi yake na mapato yake. Kila mtu anayeangalia au kuahiza bidhaa kwa njia ya intaneti anaacha habari juu yake na habari hizi zote zinakusanywa na kutumiwa kuteua watu watakaotumwa matangazo maalumu.
Mara nyingi tovuti zinazoomba watumiaji kuacha anwani ya baruapepe hukusanya data hizi ambazo mara nyingi juuzwa. Mikusanyiko wa anwani zinaweza kuwa na majina mamilioni.
Makampuni ziazokusanya data hutumia mbinu mbalimbali kujua kama anwani fulani bado ni hai yaani kama bado inatumiwa na mtu. Hapa wanajaribu kupata jibu, kwa mfano wa kuwaambia wapokeaji watume jibu kama hawataki tena kupokea uhumbe. Njia nyingine ni kuingiza picha ndogo na kama mpokeaji anabofya kuona picha mtumiaji anapata habari picha hii imefunguliwa kutoka anwani fulani.
Kuzuia spam
haririSi rahisi kuepukana na spam kabisa lakini kuna njia za kupunguza. Njia mojawapo ni kutumia anwani mbadala kwa jina tofauti. Programu za baruapepe huwa na filta na mtumiaji anaweza kuainisha ujumbe fulani kama "spam" na hivyo kuzuia anwani ya mtumiaji; habari za spam inayotambuliwa zinaweza kulengwa katika folda ya pekee ambako zinafutwa baada ya muda unaoamuliwa na mwenye akaunti.
Spam kwenye intaneti
haririSpam inatokea pia kwenye tovuti za intaneti. Hasa pale ambako wauzaji wanaficha matangazo yao kwenye ujumbe wa mitandao ya kijamii.
Makampuni makubwa kama Google, Facebook na Amazon yote yote hukusanya data za watumiaji wao[3].
Makampuni haya hayauzi data moja kwa moja kwa makampuni ya ya nje lakini yanauza matumizi ya data za watumiaji wao ili kuwalenga kikamilifu zaidi kwa matangazo ya kibiashara yanaoyonekana wakati wa kutembea tovuti mbalimbali. Imejulikana pia kuwa Facebook na Amazon na wengine wamewahi kubadilishana data zao kwa kusudi hilohilo, bila kuwaambia wateja wao[4].
Spam kwenye wikipedia
haririKuna pia spam ya viungo (ing. backlinks) kwenye wikipedia. Hapo wauzaji wanaficha matangazo kwenye viungo vya maelezo na marejeo katika makala ya wikipedia. Mbinu huu ni marufuku kwenye wikipedia na watumiaji wengiw anajitolea kutafuta marejeo ya aina hii na kuyafuta.
Marejeo
hariri- ↑ Spam - Monty Python's Flying Circus
- ↑ Blogu kuhusu asili ya neneo spam ya Brad Templeton, aliyekuwa mmoja wa waanzilishaji wa intaneti
- ↑ Are you ready? Here is all the data Facebook and Google have on you, Dylan Curran kwenye tovuti ya The Guuardian UK mnamo 2018
- ↑ Facebook didn’t sell your data; it gave it away in exchange for even more data about you from Amazon, Netflix, Spotify, Microsoft, and others, Alexis C. Madrigal Dec 19, 2018 kwenye jarida The Atlantic
Viungo vya nje
hariri- 1 December 2009: arrest of a major spammer
- Anti-Spam Consumer Resources and Information
- Cybertelecom:: Federal spam law and policy Archived 19 Julai 2019 at the Wayback Machine.
- Federal Trade Commission page with spam reduction tips and reporting
- Malware City - The Spam Omelette BitDefender’s weekly report on spam trends and techniques.
- Reaction to the DEC Spam of 1978 Overview and text of the first known internet e-mail spam.
- Slamming Spamming Resource on Spam
- Spamtrackers SpamWiki: a peer-reviewed spam information and analysis resource.
- Why am I getting all this spam? CDT