Stronti ni elementi na metali ya udongo alikalini yenye namba atomia 38 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 87.62. Alama yake ni Sr. Jina lahusiana na kijiji cha Strontian katika Uskoti ilipotambuliwa mara ya kwamza mwaka 1787.

Stronti (Strontium)
Jina la Elementi Stronti (Strontium)
Alama Sr
Namba atomia 38
Mfululizo safu Metali za udongo alikalini
Uzani atomia 87.62 u
Valensi 2, 8, 18, 8, 2
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1050 K (777 °C)
Kiwango cha kuchemka 1655 K (1382 °C)

Kama metali ya udongo alikalini zote stronti humenyuka haraka na haitokei kiasili kama elementi tupu bali katika umbo la kampaundi zake. Ikisafishwa na kutunzwa katika angahewa ya gesi adimu ni metali laini kushinda kalisi yenye rangi nyeupe-fedha. Unga wa stronti huwaka pekee yake hewani kwa moto nyekundu.

Matumizi

hariri

Matumzi yake ni hasa katika televisheni inapokorogwa katika bilauri ya tubu kwa kusidi la kuzuia kutoka kwa miali X (eksirei).

Kuna matumizi mengine kama aloi kwa mfano katika alumini.

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stronti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 1