Tako la bara
Tako la bara (ing. continental shelf) ni sehemu ya bara iliyoko chini ya maji ya bahari. Sehemu ya bahari hadi ya kina cha maji cha mita 200 huitwa "bahari ya takoni". Kwa wastani lina upana wa 70 – 80 km. Lakini kuna matako yenye upana wa kilomita zaidi ya 1,000 kama huko Siberia au nyembamba sana kama huko Kenya.
Kanda hili la tako lazungusha kila bara. Katika historia ya dunia sehemu hizi ziliwahi kuwa nchi kavu katika vipindi ambako hali ya hewa ilikuwa baridi zaidi na kiasi kikubwa cha maji cha bahari kuwa barafu nchani.
Tako la bahari kwa kawaida huishia kwenye mtelemko ambako sakafu ya bahari unatelemka chini kwa vilindi vya bahari.
Tako la bahari ni muhimu kibiolojia, kiuchumi na kisiasa.
Biolojia ya tako la bara
haririBahari ya takoni ni eneo ambako samaki wengi wanazaa kuna uwingi wa aina pia wa mimea ya bahari.
Uchumi wa tako la bara
haririKiuchumi tako la bahari ni eneo ambako malighafi ya msingi wa bahari zinapatikana. Sehemu kubwa ya mafuta ya petroli yamepatikana kwenye bahari ya takoni.
Siasa za tako la bara
haririKisiasa tako la bara limekuwa muhimu katika ushindi kati ya mataifa. Hapo nchi zimeanza kudai ya kuwa tako la bara mbele ya mwambao wao ni eneo lao chini ya maji. Kwa mfano katika fitina kati ya China na Japani kuhusu Visiwa vya Senkaku China yadokeza ya kuwa visiwa viko kwenye tako la bara linaloelekea kutoka China bara.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tako la bara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |