Thales
Thales wa Mileto (mnamo 624 KK - 546 KK [1]) alikuwa mwanafalsafa wa Ugiriki ya Kale kabla ya Sokrates. Alitokea Mileto huko Asia Ndogo.
Wengi, hasa Aristoteli, walimwona kama mwanafalsafa wa kwanza katika mapokeo ya Kigiriki. [2] Hata Bertrand Russell alisema juu yake "falsafa ya Magharibi huanza na Thales". [3]
Thales alijaribu kueleza matukio asilia bila kurejelea mytholojia au dini na alikuwa na ushawishi mkubwa. Takriban wanafalsafa wengine wote waliomtangulia Sokrates walimfuata wakijaribu kutoa maelezo kuhusu mata ya Dunia, mabadiliko, na kuwepo kwa ulimwengu — bila kurejelea mitholojia. Hatimaye kukataa kwa Thales kutafuta maelezo ya kimitholojia kukawa msingi muhimu kwa kutokea kwa sayansi. Hivyo aliitwa baadaye "Baba wa Sayansi", ingawa labda Demokrito anastahili zaidi jina hilo. [4] [5]
Katika hisabati, Thales alitumia jiometri kutatua matatizo kama vile kukokotoa urefu wa piramidi na umbali wa meli kutoka ufukweni. Yeye ndiye mtu wa kwanza anayejulikana ambaye uvumbuzi wa hisabati umehusishwa naye ambao ni uhakiki wa Thales kuhusu pembetatu mraba. Pia, Thales alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kuwa alisoma umeme.
Marejeo
hariri- ↑ tarehe halisi hazijulikani
- ↑ Aristotle Metaphysics. Alpha, 983b18.
- ↑ Russell, Bertrand (1945). The history of western philosophy. New York: Simon and Schuster.
- ↑ Singer, C. (2008). A short history of science to the 19th century. Streeter Press. uk. 35.
- ↑ Needham, C. W. (1978). Cerebral logic: solving the problem of mind and brain. Loose Leaf. uk. 75. ISBN 0-398-03754-X.
[[Jamii:{{ #if:624 KK|Waliozaliwa 624 KK|Tarehe ya kuzaliwa