"The Thunder Rolls" ni wimbo uliotolewa na msanii wa Muziki wa Country wa Marekani Garth Brooks. Iliingia uwanjani katika albamu yake ya pili No Fences na pia ikaonekana katika albamu zake The Hits, The Limited Series na Double Live. "The Thunder Rolls" ulitungwa na Garth Brooks akishirikiana na Pat Alger na ulikuwa wimbo wa sita wa Brooks ulioongoza (nafasi ya kwanza) katika chati za country[2].

“The Thunder Rolls”
“The Thunder Rolls” cover
Single ya Garth Brooks
B-side "Wolves" (The Netherlands)
"Victim of The Game" (US 7")
Imetolewa Aprili 1991[1]
Urefu 3:42
Studio Capitol Nashville 44727
Mtunzi Pat Alger
Garth Brooks

Mwanzoni ulirekodiwa na Tanya Tucker, lakini haukutolewa hadi ulipoonekana katika albamu yake ya jina hilo mnamo 1995. Toleo lake lilishirikisha ubeti wa tatu ambao Brooks mwenyewe aliazimia kuutumia katika toleo lake lakini hakufanya hivyo kulingana na ushauri wa mtayarishi Allen Reynolds.

Kuhusu Wimbo

hariri
  • Urefu: 3:42
  • Key: D Minor

"The Thunder Rolls" unasimulia hadithi ya mke ambaye anangoja hadi usiku wa manane ili mumewe aje nyumbani. Anapoingia nyumbani, mkewe ananusa manukato ya mwanamke mwingine katika nguo za mumewe. Tukio hili linatendeka wakati wa dhoruba, kama ishara ya masaibu ya ndoa hii.

Awali wimbo huu ulikuwa na ubeti wa tatu ambapo mke huyu anakimbilia kabati lake la nguo ili kuchukua bunduki, akijiambia kuwa kamwe hatakuwa akijiuliza tena mumewe yuko wapi. Hata hivyo, mtayarishi wake Allen Reynolds alionelea kuwa wimbo huu ungekuwa bora zaidi na beti za kwanza mbili na hivyo toleo la studio halikuwa na ubeti wa tatu, ingawa Brook huwa anauimba katika tamasha, inavyodhibitishwa katika albamu ya Double Live. Pia redio nyingi zilikataa kuucheza na ubeti wa tatu kwa madai kuwa ubeti huo ulichochea vita vya kinyumbani, jambo lililopelekea kukua kwake kwa kiwango katika muziki wa Country.

Video ya muziki ya wimbo huu, iliyoelekezwa na Bud Schaetzle, ilikuwa ya kwanza kabisa kurushwa hewani katika masafa ya redio ya Great American Country network. Ilipigwa marufuku kutoka CMT na TNN kwa uonyeshaji wake wa Vita vya Kijamii. Mke katika video hii anapewa jicho jeusi kutoka kwa mume asiye mwaminifu, tukio ambalo mwanao anashuhudia.

Video ya Single haina onyesho ambapo mke anaua mume (ambalo limechezwa na Brook), huku yeye na bendi yake wakichezea nje ya nyumba yao katika mvua. Kuna maonyesho mengine ambayo yanaashiria kuwa ndoa yao imekumbwa na vita tangu jadi, kwa hivyo kumpa mwanamke nia mbaya zaidi kuliko ilivyokusudiwa na wimbo.

Video hii ilishinda tuzo la ‘’Video ya Muziki ya MWaka’’ mnamo 1991 katika tamasha za CMA Awards.

Mpangilio wa Vibao

hariri

US 7" single" Capitol Nashville NR-44727, 1991

  1. "The Thunder Rolls" (iliyo haririwa) - 3:30
  2. "Victim of the Game"

Jukebox 7" single Liberty S7-57744-A, 1992

  1. "The Thunder Rolls" - 3:42
  2. "Shameless"

Dutch promo CD single Liberty/EMI promo CX 519443, 1991

  1. "The Thunder Rolls" - 3:43

Nafasi Katika Chati

hariri
Chart (1991) Peak
position
U.S. Billboard Hot Country Singles & Tracks 1
Canadian RPM Country Tracks 1

Vidokezo

hariri
  1. Garth Brooks singles at LP Discography.com link
  2. Whitburn, Joel (2004). The Billboard Book Of Top 40 Country Hits: 1944-2006, Second edition. Record Research. uk. 54.
Alitanguliwa na
"If the Devil Danced (In Empty Pockets)"
ya Joe Diffie
Billboard Hot Country Singles & Tracks
Single ya kwanza

22 Juni-29 Juni 1991
Akafuatiwa na
"Don't Rock the Jukebox"
ya Alan Jackson
Alitanguliwa na
"Meet in the Middle"
ya Diamond Rio
RPM Country Tracks
Single ya kwanza

29 Juni-13 Julai 1991
Akafuatiwa na
"Point of Light"
ya Randy Travis
Alitanguliwa na
"Hard Rock Bottom of Your Heart"
ya Randy Travis
RPM Vibao vya Country
Single ya kwanza ya mwaka

1991
Akafuatiwa na
"Achy Breaky Heart"
ya Billy Ray Cyrus
  NODES
chat 3