Tikhon wa Moscow (kwa Kirusi: Тихон Московский; jina la awali: Василий Иванович Беллавин, Vasily Ivanovich Bellavin; Klin, 31 Januari 1865Moscow, 7 Aprili 1925) alikuwa mmonaki, halafu askofu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi. Tarehe 5 Novemba 1917 alichaguliwa kuwa Patriarki wa 11 wa Moscow na Urusi wote, wa kwanza baada ya miaka 300 ya Kanisa hilo kuongozwa na Sinodi tu.

Picha halisi ya Mt. Tikhon, Patriarki wa Moscow na Urusi wote.

Mwaka 1989 alitangazwa na Kanisa lake kuwa mtakatifu, na anaheshimiwa hivyo na Waanglikana wa Marekani pia, alikowahi kufanya kazi ya umisionari.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  NODES