Ufizi wa meno (kwa Kilatini gingiva; kwa Kiingereza gum) ni tishu laini inayofunika mataya ndani ya kinywa.

Nafasi ya ufizi wa meno katika muundo wa jino

Inaziba hasa nafasi kati ya kizizi cha jino na kitundu cha taya.

Tofauti na tishu laini ya midomo na mashavu, ufizi unashikana na mfupa wa mataya chini yake.

Ufizi ulio mzima unaonyesha kwa kawaida rangi ya waridi lakini kwa watu wenye ngozi nyeusinyeusi inaweza kuwa pia na kiwango cha melanini.

Kutokea kwa madoa nyekundu, nyeupe na buluu ni alama ya magonjwa yanayohitaji kuangaliwa na daktari wa meno.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufizi wa meno kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES