Usultani wa Adal (Kisomali: Adaal, Kige'ez: አዳል ʾAdāl, Kiarabu: عدل; c. 1415 - 1555) ulikuwa dola la Kiislamu miaka 1415 hadi 1577 katika maeneo ya Ethiopia ya mashariki, Jibuti na Somaliland ya leo. Katika kipindi cha juu cha uwezo wake, Adal ilitawala sehemu kubwa za maeneo ya Ethiopia na Somalia.[1]

Maghofu ya Zeila, Somalia iliyokuwa bandari kuu ya Adal.

Vyanzo

hariri

Adal ilifuata kipindi cha Usultani wa Ifat. Baada ya usultani huo wa Kiislamu kushindwa kabisa na ufalme wa Ethiopia mnamo mwaka 1415, sehemu ya familia ya watawala chini ya Haqq ad-Din II walihamia maeneo ya Harar na Hargeisa walipoanzisha Adal. Mji mkuu wa kwanza ulikuwa Dakkar uliofuatwa baadaye na Harar.

Makabila

hariri

Wakazi wa sehemu hizo na pia askari wa jeshi lake walikuwa hasa Wasomali na Waafar.[2] Viongozi wake, hasa Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi au Ahmad Gran, walitazamwa kama Wasomali. [3]

Eneo la Ethiopia

hariri

Tangu mwaka 1288, Adal ilikuwa eneo la Waislamu. Eneo la mtawala wa Kikristo wa Ethiopia aliyeitwa wa nasaba ya Solomoni. Muda mfupi, baadae eneo hili lilipiganiwa na kuwa chini na Ethiopia. Negus Negesti Amda Seyonna kampeni zake za mwaka 1332. Katika kipindi hiki, Mfalme wa Shewa Na Mfalme wa Ifat waliokuwa wakiongoza misafara ya kibiashara na bandari katika mwambao wa , pamoja na mfalme wa Zeila pia walitekwa.Baadae Adal ilikuja kuongozwa na Ifat, lakini baadea ilikuja kuwa huru baada ya mapigano yake dhidi ya Amde Seyon, lakini baadae tena, walijisalimisha baada ya Mfalme wao kufariki na kutekwa kwa mji mkuu wao wao Talag Na huo ndio ukawa mwisho Jamal ad-Din wa Ifat na ufalme wake. [4]

Katika mwaka kati ya 1403 au 1415, Waethiopia walivamia tena Ifat ambayo ndio tu ilikua imetoka katika mapigano, na kuweza kuwapiga maadui zao chini ya Mfalme wao. Sa'ad ad-Din II. Sa'ad ad-Din alifukuzwa kutoka katika utawala wao na ufalme wa Ethiopia, hii ikiwa ni mwaka 1403 au Yeshaq I in 1415) na baadae kuvamia eneo la Zeila na kumuua. Matokeo yake Familia za matajiri waliondoka nchini humona kukimbilia nchini Yemen kuepuka kukamatwa na kuuwawa. Walipokuja kurejea, walikuta tayari ufalme umebadilishwa kutoka jina la Mfalme wa Ifat na kuwa Mfalme Adal hii ikionesha kuwa, Ifat ilikuwa sehemu ya Adal.

Kuvamiwa kwa Ethiopia

hariri

Katika miaka ya katika ya 1520 Imam Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi Aliivamia Adal na kutangaza rasmi vita takatifu dhidi ya wakristu wa Ethiopia.ambao kwa wakati huo walikuwa chini ta utawala wa Lebna Dengel. Wakiwa wanapewa zana za kupigania kutoka katika Ufalme wa Ottoman,. Ahmad aliweza kuwapiga waethiopia katika vita vya Battle of Shimbra Kure mwaka 1529, na kuweza kuchukua mali zote kutoka Ethiopia, kama vile maeneo ya mwinuko, japokuwa waethiopia waliendelea kukataa kuachia maeneo hayo. Mwaka 1541, Ureno ambayo ilikuwa wakihitaji baadhi ya maeneo katika Bahari ya Hindi, walituma msaada wa askari kwa Waethiopia. Na kwa kujibu suala hilo, Adal nao wakapokea askari 900 kutoka katika ufalme wa Ottomans

Imam Ahmad aliweza kufanikiwa katika mapigano dhidi ya Waethiopians, wakati akiendelea na kampeni katika Autumn mwaka 1542. Aliweza kumuua kiongozi wa kijeshi wa Ureno, Cristóvão da Gama mwezi Agosti mwaka huo huo. Hatahivyo wapiganaji wa Kireno walikataa kujisalimisha kutokana na kifo cha Adal katika vita vya Battle of Wayna Daga, karibu na ziwa Tana mwezi Februari mwaka 1543, ambapo Ahmad aliuwawa katika vita hivyo. Kutokana na hali hiyo, Waethiopia waliweza kuchuakua uwanda wa juu ulioinuka walioupateza baada ya kushindwa katika vita dhidi ya Adal. Mwaka 1577, mji mkuu wa Adal na uliamishiwa kutoka Zeila na kwenda Harar n hii ilifuatia kuanguka kwa utawala wa Adal.

Marejeo

hariri
  1. Travis J. Owens: Beleaguered Muslim fortresses and Ethiopian imperial expansion from the 13th to the 16th century, June 2008 Monterey, CA 93943-5000 (M.A. Thesis), [https://apps.dtic.mil/dtic/tr/fulltext/u2/a483490.pdf online hapa]
  2. Herausgegeben von Uhlig, Siegbert, Encyclopaedia Aethiopica. Wiesbaden:Harrassowitz Verlag, 2003, pp.71
  3. ibid, pp. 155
  4. ibid, pp.71

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usultani wa Adal kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES