Utumiaji mbaya wa vileo

(Elekezwa kutoka Utumiaji mbaya wa Pombe)

Utumiaji mbaya wa vileo ni uraibu unaoelekeza kutumia mara kwa mara vileo licha ya madhara yake. Unatofautiana na utegemezi wa pombe kwa ukosefu wa dalili kama vile kuvumilia na uondoaji. Hata hivyo, maana nyingi za ulevi zipo, na ni baadhi tu zilizo sambamba na utumiaji mbaya wa pombe.

Tiba kwa Utumiaji Mbaya wa Pombe inatofautiana, lakini kuna mipango kadhaa inayotumika kutoka kwa uzuiaji hadi vituo maalumu kulingana na umri na jinsia. Mara nyingi kuna unyanyasaji wa kimwili unaohusiana na ulevi. Mipango ya matibabu kwa vikundi inayojumuisha wanawake pekee, kwa mfano, inaweza kusaidia kutatua masuala yanayozunguka wanaume waathirika. Vituo vya urekebishaji vinapendekezwa kwa kuondoa kemikali kwani kunaweza kuwa na madhara makubwa ya kimwili, pamoja na mauti, isipotibiwa vyema.

Unyuaji chuoni Marekani

hariri

Utafiti wa mwaka 2001 ulionyesha "asilimia 29 ya wanafunzi wa vyuo Marekani wameendesha gari wakiwa chini ya ushawishi wa pombe'" (Windel). Matokeo ya utafiti tofauti uliofanywa yalikuwa "wanafunzi milioni 2.1 kati ya umri wa miaka 18 na 24 waliendesha gari chini ya ushawishi wa pombe'" (serikali ya Marekani). Matokeo hayo yanaonyesha vile ulevi na uendeshaji gari chuoni lilivyo suala kubwa. Ripoti ya mwaka wa 1995 ya Centers for Disease Control and National College Risk Behavior Survey iliaarifu juu ya "asilimia 39.9% ya wanafunzi walevi katika mwezi uliopita" (Beck).

Marejeo

hariri
  • National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism. "Diagnostic Criteria for Alcohol Abuse and Dependence" Alcohol Alert, No. 30 PH 359, Oktoba 1995.
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utumiaji mbaya wa vileo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES