Wakelti walikuwa watu wa kundi kubwa la makabila ya Ulaya katika Zama za Kale.

Uenezi wa Wakelti wa kale:
     Eneo la Utamaduni wa Hallstatt mnamo karne ya 6 KK      Uenezi mkubwa zaidi wa Wakelti mnamo mwaka 275 KK      Eneo la Lusitania kwenye rasi wa Iberia ambako hakuna hakika juu ya kuwepo kwa Wakelti      Maeneo ambako wasemaji wa lugha za Kikelti walibaki hadi mwisho wa Zama za Kati      Maeneo yenye wasemaji wa lugha za Kikelti hadi leo
Sanaa ya Wakelti: Bakuli la fedha kutoka Gundestrupp, Denmark

Jina linatokana na taarifa za Wagiriki wa Kale, waliowaita Κέλτοι Keltoi au Γαλάται Galatai, na za Waroma wa Kale waliowaita Celti. Wenyewe hawakuacha maandishi, kwa hiyo haijulikani kama walikuwa na jina la kujiita kwa jumla.

Walitumia lugha za karibu. Leo hii wasemaji wasio wengi wa lugha hizo wamebaki Uingereza, Eire na Ufaransa ambao ni wasemaji wa Kibretoni, Kicornwall, Kiwelisi na Kigaelic.

Pamoja na hayo, wataalamu wa akiolojia wametambua mabaki ya kufanana ambayo yanahesabiwa kuwa ya Wakelti kutokana na makaburi, makazi, vifaa vya ufinyanzi, mapambo ya silaha na kadhalika yanayoruhusu kuelewa uenezi wao, hata kama hakuna taarifa za kimaandishi ya majirani.

Kutokana na makaburi yaliyochunguzwa huko Hallstadt / Austria, jina la "utamaduni wa Hallstatt" likabuniwa. Wakubwa wa utamaduni huo walizikwa pamoja na silaha zao zilizochongwa na kupambwa kwa namna ya pekee na aina hizi za vifaa makaburini zimetambuliwa pia mahali pengine.

Taarifa zaidi zinapatikana katika maandiko ya Wagiriki na Waroma wa Kale waliofanya biashara na makabila ya Wakelti na kupambana nao katika vita. Julius Caesar alitunga taarifa yake juu ya "De bello gallico" (yaani "Vita vya Gallia") ambako aliingiza maelezo mengi juu ya jamii, utamaduni, uchumi na dini ya Wakelti wa Gallia aliowashinda.

Asili na uenezi

hariri

Asili yao inaaminiwa kuwepo upande wa kaskazini wa milima ya Alpi.

Walikalia funguvisiwa ya Britania, sehemu za Ulaya ya Magharibi, ya Kati na ya Mashariki. Hapo walikuwa na nguvu hasa katika Gallia ya kihistoria (leo Ufaransa, Ubelgiji na Italia ya Kaskazini).

Makabila kadhaa yalihama hadi Anatolia (Uturuki wa leo).

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakelti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 1