Wangwa wa Lagos uko nchini Nigeria ukiwa mmojawapo kati ya nyangwa kubwa kwenye pwani ya ghuba ya Guinea. Eneo lake ni takriban km² 6,354.7[1]

Ramani ya sehemu ya magharibi ya Wangwa wa Lagos

Ni gimba la maji lenye urefu wa kilomita 60 na upana hadi km 15. Kina cha wastani ni mita 2 pekee. Maji yake ni mchanganyiko wa maji ya bahari na maji ya mito hivyo yana chumvi kidogo tu. Mito ya Ogun na Osun inaishia hapa.

Ufuko wa wangwa una misitu ya mikoko inayotumika kwa ufugaji wa samaki. Machafuko wa maji ni tatizo kubwa kwa sababu maji machafu kutoka mji na viwanda yanaingia humo bila kusafishwa.

Bandari ya Lagos iko ndani ya wangwa. Beseni zake pamoja na njia ya kuingia baharini vinapaswa kuchimbwa mara kwa mara kwa kutunza kina cha kutosha kwa meli kubwa.

Marejeo

hariri
  1. Lagos Lagoon Coastal Profile: Information Database For Planning Theory, by Obafemi McArthur Okusipe, Department of Urban and Regional Planning, University of Lagos - Accessed September 22, 2008
  NODES