Watakatifu wote (kwa Kigiriki: Αγίων Πάντων, Agiōn Pantōn) ni sherehe ya liturujia katika madhehebu mengi ya Ukristo[1][2][3][4][5] inayoadhimishwa tarehe 1 Novemba katika Kanisa la Kilatini[6] na madhehebu kadhaa ya Uprotestanti.

Watakatifu wote katika mchoro wa Fra Angelico.

Desturi hiyo ya Ukristo wa magharibi inatokana na kwamba katika mwaka wa Kanisa mwezi Novemba ni wa mwisho, hivyo umeonekana unafaa kuutumia kutafakari juu ya mambo ya mwisho: kifo, hukumu, moto na mbingu. Watakatifu ni watu wanaosadikiwa wamekwishaingia pamoja na Kristo katika utukufu wa Paradiso walau kwa roho yao, kama mhalifu aliyetubu karibu na Yesu msalabani.

Kumbe katika Ukristo wa mashariki huadhimishwa Jumapili ya kwanza baada ya Pentekoste, ili kusisitiza uhusiano wa utakatifu wa binadamu na Roho Mtakatifu. Ni yeye tu anayewawezesha kushinda dhambi katika maisha yao.

Walengwa wa heshima hiyo, baada ya Mungu aliyewatakasa kwa njia ya Yesu Kristo, ni watakatifu wote, wanaojulikana na wasiojulikana sawia.

Kwa shangwe moja, Kanisa linalosafiri bado duniani linaheshimu wale wote wanaopongezwa mbinguni, ili lichochewe na mfano wao, lifurahie ulinzi wao na lijione limetiwa na Mungu taji la ushindi wa milele[7].

Ingawa kila mtakatifu anakumbukwa siku maalumu ya mwaka, sikukuu hii ya pamoja inasisitiza uzuri wa umoja wao mbinguni, pamoja na wingi wao, kama ulivyosisitizwa na Mtume Yohane katika kitabu cha Ufunuo. Hivyo ni chanzo cha tumaini jipya kwa binadamu wanaosafiri bado duniani kuelekea huko kati ya majaribu mengi.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Roman Missal
  2. St. John of Shanghai and San Francisco. "Homily on the Feast of All Saints of Russia". St. John Chrysostom Orthodox Church.
  3. The Anglican Service Book. Good Shepherd Press. 1 Septemba 1991. uk. 677. ISBN 0962995509. Iliwekwa mnamo 3 Novemba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Marty, Martin E. (2007). Lutheran questions, Lutheran answers: exploring Christian faith. Minneapolis: Augsburg Fortress. uk. 127. ISBN 978-0-8066-5350-1. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2011. All Lutherans celebrate All Saints Day, and many sing, 'For all the saints, who from their labors rest…'{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Willimon, William H. (2007). United Methodist Beliefs. Westminster John Knox Press. uk. 64. ISBN 9781611640618. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2014.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Martyrologium Romanum
  7. https://www.santiebeati.it/dettaglio/20500

Marejeo

hariri
  • Langgärtner, Georg. "All Saints' Day". In The Encyclopedia of Christianity, edited by Erwin Fahlbusch and Geoffrey William Bromiley, 41. Vol. 1. Grand Rapids: Wm. B. Eerdmans, 1999. ISBN 0802824137.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watakatifu wote kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES