Watrapisti (ufupisho wa jina la shirika lao ni OCSO, Ordo Cistercensium Strictae Observantiae) ni wamonaki wa Kanisa Katoliki wanaofuata kikamilifu urekebisho wa umonaki wa Kibenedikto ambao ulianza Citeaux (leo nchini Ufaransa) tarehe 21 Machi 1098 ukaenea haraka kila mahali katika karne ya 12, hasa kutokana na mvuto wa mwanashirika Bernardo wa Clairvaux.

Abasia ya Citeaux.

Jina linatokana na monasteri ya La Trappe, Normandy, ambapo mwaka 1664 Armand Jean le Bouthillier de Rancé alianzisha tapo lenye msimamo mkali zaidi kuhusu kazi za mikono, kimya, kujinyima chakula, kujitenga na ulimwengu na kukataa masomo mengi.

Kwa sasa (2018) wana monasteri 168 katika mabara yote.

Wasitoo wengine wanaunda shirikisho la O.Cist..

Marejeo

hariri
  • Plouvier, M. and Saint-Denis, A. (eds.), 1998: Pour une histoire monumentale de Cîteaux, 1098-1998 (Commentarii cistercienses. Studia et documenta, 8), Cîteaux.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Picha za Citeaux

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watrapisti kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
mac 2
os 1
web 1