Wayne Rooney

Mchezaji mpira na meneja wa Uingereza

Wayne Rooney alikuwa mchezaji wa kandanda aliyeichezea hasa timu ya Manchester United.

Rooney akiichezea Manchester United mwaka 2016.

Amezaliwa tarehe 28 Oktoba 1985 katika mji wa Liverpool katika nchi ya Uingereza.

Alichezea timu ya taifa ya Uingereza katika kombe la dunia mwaka wa 2006 akiwa na umri wa miaka 21. Inasemekana kuwa Rooney aliwahi kupitia mafunzo ya bondia kabla ajiunge na soka. Baada ya kuachana na Man United alihamia katika klabu cha Everton na kuichezea mechi yake ya kwanza dhidi ya Gormahia ya Kenya katika finali ya michezo ya sportpesa huko nchini Tanzania na kufunga bao. Mchezaji huyo alikuwa anavaa jezi namba 10 na kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Mchezaji huyo alilipwa mshahara mkubwa kuliko wote Uingereza, kiasi cha paundi 300,000 kwa wiki.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wayne Rooney kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
os 1