"We Are the World" ni wimbo wa hisani uliorekodiwa na kundi bab-kubwa la USA for Africa kunako mwaka wa 1985. Wimbo ulitungwa na Michael Jackson na Lionel Richie na kutayarishwa na Quincy Jones na Michael Jackson kwa ajili ya albamu ya We Are the World. Kwa mauzo yaliyozidi kiasi cha nakala milioni 20, ni moja kati ya single chache mno kuuza nakala milioni 10 (au zaidi) kwa dunia nzima.

We Are the World
“We Are the World” cover
Single ya USA for Africa
kutoka katika albamu ya We Are the World
B-side Grace
Imetolewa 7 Machi 1985
Muundo 7", 12"
Imerekodiwa 28 Januari 1985
A&M Recording Studios
(Los Angeles, California)
Aina Pop, gospel
Urefu 6:24 (7" Version)
7:09 (12" Version)
Studio Columbia
Mtunzi Michael Jackson
Lionel Richie
Mtayarishaji Quincy Jones
Michael Omartian
Certification 4× Platinum (RIAA)

Kufuatia mradi wa Band Aid, "Do They Know It's Christmas?" huko nchini Uingereza, wazo la uanzishaji wa kibao cha kusaidia balaa la njaa barani Afrika linatoka kwa mwanaharakati Harry Belafonte, yeye, akiwa na mchangishaji fedha Ken Kragen, walikuwa chombo kikuu katika kuleta wazo hili katika hali ya ukweli. Wanamuziki kadhaa waliitwa wakiwa wawiliwawili, kabla Jackson na Richie kupewa kazi ya kutunga wimbo.

Kufuatia miezi kadhaa ya kufanya kazi pamoja, wawili hao walimaliza kabisa kazi ya utunzi wa "We Are the World" usiku mmoja kabla ya hatua ya kwanza ya kurekodi wimbo huo, mwanzoni mwa mwaka wa 1985. Hatua ya mwisho ya kurekodi wimbo huu ulimalizika mnamo tar. 28 Januari 1985. Tukio hili la kihistoria limewaleta pamoja baadhi ya wasanii mashughuli katika tasnia ya muziki kwa kipindi hicho.

Wimbo ulitolewa kunako tar. 7 Machi 1985, ikiwa kama single pekee kutoka katika albamu. Mafanikio kedekede duniani kote, imeshika chati za juu katika nchi kibao duniani na kuufanya uwe wimbo pekee wa pop kuuzika haraka sana katika historia ya muziki huo kwa nchini Marekani. Single ya kwanza kutunukiwa maplatinamu kedekede, "We Are the World" imepokea platinamu nne mfululizo kutoka kwa Recording Industry Association of America.

Hata hivyo, wimbo umepokea tahakiki mchanganyiko kutoka kwa waandishi wa habari, wataalamu wa muziki, na jamii kwa ujumla. Mashabiki wamefurahi kusikia muziki ulioimbwa pampoja na watu wa rangi tofauti katika wimbo mmoja, na kujisikia raha kununua "We Are the World", wakitambua ya kwamba pesa zinaenda katika jambo la hisani. Wengineo, wakiwemo wasemaje wa vyombo ya habari, walikatishwa tamaa eti kwamba wimbo haujatoa sababu kwa wasikilizaji kwanini njaa imetokea mwanzoni kabisa, na mashairi yalionekana kama vile ya kujipatia umaarufu tu.

Wimbo umezawadiwa tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na Grammy Awards tatu, moja American Music Award, na People's Choice Award—wimbo ulipandishwa na upokeaji wa tahakiki za haja za video yake, video za nyumbani, na matoleo ya vijarida, na matangazo kibaokibao ya redio, TV, na kadhalika, vitabu, mabango, na fulana. Promosheni yake imesadia mafanikio ya "We Are the World" na kuchangisha kiasi cha pesa zaidi ya Dola za Kimarekami Milioni 63 kwa ajili ya shughuli kusadia watu barani Afrika na Marekani.

Kufuatia uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa magnitude 7.0 M huko nchini Haiti mnamo tar. 12 Januari 2010, toleo lingine la wimbo huu na mastaa wengine lilitolewa na -rekodiwa mnamo 1 Februari 2010. Wimbo uliitwa jina la "We Are the World 25 for Haiti", ulitolewa kama single mnamo tar. 12 Februari 2010, na mapato kutoka katika rekodi hiyo ilisaidia walioponyeka katika nchi iliyopatwa na balaa hilo.

Wanamuziki wa USA for Africa

hariri
Mwelekezaji

Waimbaji (kulingana na mwonekano katika video)

Kiitikio (kiherufi)

Bendi

Orodha yake

hariri

Vinyl Single:

  1. "We Are the World" – 7:09

VHS Video Event 1:

  1. "We Are the World" – 7:09
  2. "Dancin' in the Street"

VHS Video Event Special Edition:

  1. "MusicVision Logo/We Are the World" – 7:27
  2. "We Are the World: Behind the Scenes"
  3. "Michael Jackson's We Are the World Demo at the Studio"

Chati na kutunukiwa

hariri

Kigezo:Certification Table EntryKigezo:Certification Table EntryKigezo:Certification Table Bottom

Chati (1985) Peak
nafasi
Australian Kent Music Report[1] 1
Austrian Singles Chart[2] 2
Canadian RPM Adult Contemporary[3] 1
Canadian RPM Top Singles[4] 1
Dutch Top 40[5] 1
Irish Singles Chart[6] 1
French Singles Chart[2] 1
Italian Singles Chart[7] 1
New Zealand Singles Chart[2] 1
Norwegian Singles Chart[2] 1
Swedish Singles Chart[2] 1
Swiss Singles Chart[2] 1
UK Singles Chart[1] 1
US Billboard Hot 100[1] 1
US R&B Singles Chart[1] 1
US Billboard Country Singles Chart[1] 76

Mauzo na kutunukiwa

hariri

Kigezo:Certification Table Top Kigezo:Certification Table Entry Kigezo:Certification Table Entry Kigezo:Certification Table Entry

Japan (RIAJ) 311,000[8]
Total certified sales: 9,555,000

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 George, p. 41
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named Ultratop Singles Chart Archives
  3. RPM "Adult Contemporary: May 18, 1985". Library and Archives Canada. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2010. {{cite web}}: Check |url= value (help)
  4. "RPM Top Singles: May 4, 1985". Library and Archives Canada. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2010.
  5. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named WATW NL
  6. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named WATW Ireland
  7. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named WATW Italy
  8. "List of best-selling international singles in Japan". JP&KIYO. 2002. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2013-01-11.
Bibliografia

Viungo vya nje

hariri


Kigezo:Harry Belafonte Kigezo:Stevie Wonder

  NODES
Association 1
chat 6
Intern 1
iOS 2
mac 5
os 8
text 4
web 3