Mafia ni mojawapo kati ya wilaya 8 za mkoa wa Pwani katika Tanzania yenye postikodi namba 61700.

Eneo lake ni hasa Kisiwa cha Mafia na visiwa vidogo karibu nacho, likitazama mwambao wa Afrika ya Mashariki km 130 kusini kwa Dar es Salaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni km 16.

Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa km 50 na upana wa km 8; eneo lake ni takriban km² 400. Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole uliokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole karibu na kisiwa kikuu.

Mji mkubwa na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ilikuwa na wakazi wapatao 46,438 [1] walioishi humo. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 66,180 [2].

Kata za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo[3]:

Shehia Eneo
km²
Wakazi
2002
Vijiji
Baleni[4] 132.1 9137 Baleni, Kungwi, Ndagoni[5], Chunguruma
Jibondo 21.9 3405 Jibondo, Chole, Juani
Kanga 52.7 3317 Kanga, Bweni
Kilindoni 36.8 11696 Kilindoni, Dongo
Kirongwe 77.0 5260 Kirongwe, Jimbo, Banja, Jojo
Kiegeani 40.3 3379 Kiegani, Marimbani
Miburani 52.3 4363 Miburani, Mlongo, Chemchem
Wilaya ya Mafia 413 40801 20 villages

Baleni, Kanga na Kirongwe kwa pamoja ni tarafa ya kaskazini, shehia nyingine ni tarafa za kusini.

Marejeo

hariri
  1. "Sensa ya 2012, Pwani - Mafia DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-13.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. [International Resources Group: Strategic Environmental Assessment of Mafia Island, FINAL REPORT, Volume II: Main Report] (PDF)
  4. Tangu kupatikana kwa orodha hii Baleni imegagiwa na Ndagoni kuwa kata ya pekee
  5. Tangu kupatikana kwa orodha hii Baleni imegagiwa na Ndagoni kuwa kata ya pekee
  Kata za Wilaya ya Mafia - Mkoa wa Pwani - Tanzania  

BaleniJibondoKangaKiegeaniKirongweKilindoniMiburaniNdagoni


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mafia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
  NODES
Intern 1
os 1