Wimbiredio (ing. radio wave) ni sehemu ya mnururisho sumakuumeme. Ni mawimbi yenye masafa ya mawimbi (ing. wavelength) baina ya sentimita 10 na kilomita 100; upeo wa marudio ni kilohezi kadhaa hadi gigahezi 3.

Sawa na mawimbi yote ya sumakuumeme zinatembea kwa kasi ya nuru. WImbiredio hutokea kiasili kutokana na radi, au mnururisho wa nyota. Tabia ya nyota kutoa mnururisho huu inatumiwa na astronomia kwenye vituo vya pekee ambako antena kubwa zinakusanya wimbiredio kutoka anga la ulimwengu.

Jina "wimbiredio" latokana na matumizi kwa mitambo ya redio. Mnamo 1873 James Clerk Maxwell alionyesha kwa njia ya hisabati ya kwamba mawimbi sumakuumeme yanaweza kupita hewani. Heinrich Rudolf Hertz alifaulu mwaka 1888 kutengeneza mawimbi haya na kuyapokea. Hii ilikuwa chanzo cha upelekaji habari kwa njia ya wimbiredio.

  NODES